У нас вы можете посмотреть бесплатно Polisi watapakaa mitaani Mwanza wafanyabiashara wakiendeleza mgomo или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wakati mgomo wa wafanyabiashara jijini Mwanza ukiingia siku ya pili, maofisa wa Jeshi la Polisi wanaotembea na waliopo kwenye magari wameonekana wakipita katika mitaa mbalimbali ya jijini hilo, huku maduka yakiwa hayajafunguliwa. Kamera ya Mwananchi Digital iliyoko mtaani kuanzia saa 12:30 hadi saa 3:00 asubuhi ya leo Jumatano Juni 26, 2024, imeshuhudia magari yaliyojaa askari wa Jeshi la Polisi yakikatiza, huku baadhi ya askari polisi wakitembea kwa miguu kuzunguka mitaa ya jiji hilo. Alipoulizwa kuhusu askari hao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kuwasambaza askari katika mitaa ya jiji hilo, huku akidokeza kuwa jukumu lao ni kuimarisha ulinzi kwa wafanyabiashara watakaofungua maduka, ili wasifanyiwe fujo na waliogoma. Kamanda Mutafungwa amesema ulinzi na doria hizo zitakuwa endelevu hadi hali itakaporejea katika utimamu, huku akionya watakaojaribu kuwafanyia vurugu wafanyabiashara walioridhia kufungua maduka yao. (Imeandikwa na Mgongo Kaitira). #mwananchiupdates #tunaliwezeshataifa