У нас вы можете посмотреть бесплатно HALI MBAYA KWA WAKIMBIZI WA BURUNDI KIGOMA, KAMBI ZINAFUNGWA- RUDINI KWENU. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KIGOMA. KAMBI ya Wakimbizi Nduta inayohifadhi Wakimbizi wa Nchi ya Burundi, inatalajiwa kufungwa ifikapo March 31 mwaka 2026, ikiwa ni mkakati wa Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya Nchi pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR, kuchukua hatua za kuwarudisha Wakimbizi wa Burundi waliokimbia nchi yao kutokana na machafuko ya vita. Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi Wizara ya mambo ya ndan ya Nchi Tanzania Sudi Mwakibasi amesema hayo wakati akihutubia Wakimbizi wa kambi ya Nduta iliyopo Wilayani Kibondo mkoani Kigoma, na kueleza kuwa kutokana na hali ya usalama Nchini Burundi kuimalika Warundi hawana budi kuondoka Tanzania kabla ya kambi hiyo kufungwa. Amesema, wakati ukifika Wakimbizi wote watakao kaidi kurudi hawatakuwa na maeneo ya kuishi na nyumba zao zitavunjwa sambamba na kuwachukulia hatua kutokana na kukiuka kurudi kwao katika kipindi cha promosheni ya serikaili na UNHCR. Hatahivyo Balozi mdogo wa Burundi Nchini Tanzania Kekenwa Jeremia amewaomba ndugu zake kurudi kwa hiari na kuwaeleza kuwa, nchi ya Burundi iko salama na hakuna machafuko yoyote hivyo hawana budi kuungana na ndugu zao kujenga nchi yao kwa pamoja. Shirika la UNHCR linaendelea Promosheni ya uandikishaji Wakimbizi wa Burundi, waliokimbia Nchi hiyo kwa vita kuhakikisha wanarudi kwao sambamba na kuwahakikisha usalama, pindi watakapolejea. MWISHO.