У нас вы можете посмотреть бесплатно UMOJA WA BODABODA, BAJAJI NA WAJASIRIAMALI WAGOMA KUANDAMANA CHADEMA, WAFUNGUKA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Umoja wa Waendeshaji Bajaji, Bodaboda na Wajasiriamali jijini Dar es Salaam, umetangaza kutoshiriki maandamano yaliyoitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yaliyopangwa kufanyika Aprili 24, 2025, kuelekea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambako kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, inatarajiwa kusikilizwa. Makamu Mwenyekiti wa Wajasiriamali Wadogo nchini, Steven Lusinde, ametoa tamko hilo leo Ilala Jijini Dar es salaam akisisitiza kuwa wanachama wao wameamua kutumia siku hiyo kufanya kazi na kujitafutia kipato badala ya kushiriki maandamano. Aidha, alieleza kuwa kundi hilo halihusiki na vitendo vya uchochezi na badala yake linahamasisha amani. Pia alikumbusha kauli ya zamani ya kiongozi mmoja wa Chadema aliyewahi kudharau kazi ya bodaboda kwa kuitaja kuwa ni ‘kazi ya laana’, jambo ambalo limewaudhi wahusika wengi. Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Maofisa Wasafirishaji nchini, Said Kagomba, alisema kuwa walipokea taarifa kupitia vyombo vya habari kuhusu wito wa Chadema kwa wananchi kujitokeza kwa wingi mahakamani siku hiyo. Hata hivyo, alibainisha kuwa wao hawatahusika na maandamano hayo, huku akiomba mamlaka husika, hasa Jeshi la Polisi, kuchukua hatua za kuhakikisha amani inatawala.