У нас вы можете посмотреть бесплатно Bodi ya Shule Ya Sekondari Oldeani Watoa TSh 4,876,000 Kuwapongeza Walimu Baada ya Matokeo 2025 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Bodi ya Shule ya Sekondari Oldeani kwa kushirikiana na uongozi wa shule imeandaa hafla maalum ya kuwapongeza na kuwapa motisha walimu pamoja na watumishi wengine wa shule kufuatia matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne na Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili mwaka 2025. Katika hafla hiyo, walimu na watumishi wa shule walipewa motisha ya jumla ya TSh 4,876,000 kama pongezi kwa mchango wao katika kufanikisha matokeo. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mwakilishi wa Afisa Elimu wa Wilaya Lusajo Daudi Ndimbo, Afisa Elimu wa Kata ya Oldeani Solomon Mwenda, pamoja na wakuu wa shule za sekondari jirani akiwemo Emanuel Bayyo (Gyekrum Arusha Secondary School) na Elizabeth Kipandwa (Wel Wel Secondary School). Pia Fredrick Lema, Mkurugenzi wa Shirika La Rift Valley Children Fund, alihudhuria tukio hilo kama mdau wa maendeleo ya elimu. Huu ni muendelezo wa utamaduni wa Shule ya Sekondari Oldeani wa kuthamini juhudi za walimu na watumishi katika kuendeleza elimu na kuwahamasisha kuendelea kufanya kazi kwa bidii. #OldeaniSecondary #ElimuTanzania #Walimu #MatokeoYaMitihani #Education