У нас вы можете посмотреть бесплатно RC MRINDOKO AWAOMBA WANANCHI KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO KAMA KAWAIDA, ASEMA MKOA WA KATAVI UKO SALAMA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, amewahakikishia wananchi wa mkoa huo kuwa hali ya usalama imeendelea kuwa shwari na amani imetamalaki katika maeneo yote ya mkoa, hivyo hakuna sababu ya kuwa na hofu. Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, RC Mrindoko amewaomba wananchi wa Katavi kuendelea na shughuli zao za kila siku kama kawaida, ikiwemo kilimo, biashara na kazi nyingine za uzalishaji, huku akisisitiza kuwa serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhakikisha utulivu unaendelea kudumu. “Nawaomba wananchi wa Katavi muendelee na shughuli zenu za kila siku kwa utulivu. Mkoa wetu uko salama, na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vipo kazini usiku na mchana kuhakikisha hali hiyo inaendelea kuwa ya kawaida,” alisema RC Mrindoko. Ameeleza kuwa tangu kipindi cha uchaguzi kumalizika, mkoa wa Katavi umeendelea kuwa mfano wa amani na mshikamano, hali inayotokana na ushirikiano mkubwa kati ya wananchi na serikali. Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka viongozi wa maeneo, watumishi wa umma pamoja na watoa huduma za kijamii kuendelea kutoa huduma kwa wananchi katika sekta zote muhimu kama afya, elimu, maji na kilimo bila ubaguzi. Amesisitiza pia umuhimu wa wananchi kuwa makini na kutojihusisha na taarifa au propaganda zinazoweza kuleta taharuki, na badala yake kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya usalama endapo watabaini viashiria vya uvunjifu wa amani. Vilevile, RC Mrindoko amewataka wafanyabiashara kutokutumia nafasi ya changamoto zilizojitokeza katika baadhi ya mikoa mingine kama kigezo cha kupandisha bei za bidhaa na mazao, akisisitiza umuhimu wa kufanya biashara kwa uadilifu na uzalendo.