У нас вы можете посмотреть бесплатно Shule ya English Medium ya Serikali ilivyoleta mtifuano na wazazi Moshi или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi J.K. Nyerere, iliyopo Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, wameijia juu Halmashauri ya Manispaa hiyo, kwa kutaka kuwahamisha wanafunzi zaidi ya 500 bila maridhiano baada ya shule hiyo kuwa ni ya Mchepuo wa masomo ya Kiingereza. Hatua hiyo, imekuja wakati shule zikitarajiwa kufunguliwa Jumatatu Januari 8, mwaka huu ambapo wazazi wa wanafunzi hao wameeleza kitendo cha kutakiwa kuwahamisha watoto wao katika shule hiyo bila makubaliano waliyokubaliana ni kitendo cha kuwachonganisha wananchi na serikali. Hata hivyo, wazazi hao walieleza kuwa, katika kikao cha mwisho cha bodi ya shule walichokaa waliambiwa wataletewa mrejesho mapema na kwamba mpaka kufikia jana wazazi hao walipewa majibu kwa barua kwamba wanatakiwa kuondosha watoto wao shuleni hapo na wachague shule ambazo wanataka watoto wakasome. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe amesema kuhusu shule hiyo kuwa na mchepuo wa Kiingereza ilikuwa ni mchakato wa muda mrefu na kwamba hawajakurupuka na wazazi walishirikishwa.