У нас вы можете посмотреть бесплатно Historia yaandikwa Lendikinya Uzinduzi wa Maktaba mpya ya Kisasa или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Uzinduzi wa Maktaba Mpya ya Kisasa Shule ya Msingi Lendikinya Shirika la From Hearts 2 Hand limejenga na kuzinduliwa rasmi Maktaba ya Kisasa katika Shule ya Msingi Lendikinya, wilayani Monduli. Uzinduzi huu wa kihistoria uliofanyika hivi karibuni, umejumuisha viongozi wa serikali, wadau wa elimu, walimu wa shule, na wananchi ambao walikusanyika kwa wingi kushuhudia tukio hili la kipekee. Rais wa From Hearts 2 Hand, Bi. Briana Greene, aliongoza uzinduzi huu, ambapo aliwahakikishia wakazi wa Lendikinya na taifa kwa ujumla kuwa maktaba hii mpya ni mchango mkubwa katika kuboresha elimu na kuhakikisha watoto wa jamii hii wanapata fursa nzuri ya kujifunza. Alisema, “Maktaba hii itakuwa ni chimbuko la maarifa na rasilimali za elimu ambazo zitasaidia watoto wetu kufikia malengo yao ya kielimu.” Viongozi wa serikali waliokuwapo walieleza furaha yao kwa kuona uwekezaji huu mkubwa katika sekta ya elimu. Mwenyekiti wa Kijiji hicho alisisitiza kuwa, "Maktaba hii itakuwa chachu ya kuboresha ufaulu wa wanafunzi, kwani itawapa nafasi nzuri ya kupata vitabu na vifaa vya kisasa vya kujifunza." Walimu wa shule ya Lendikinya walieleza matumaini yao makubwa kwa mafanikio ya wanafunzi baada ya kujengewa mazingira bora ya kujifunzia. “Hii ni fursa adhimu kwa wanafunzi wetu. Tumekuwa tukikosa vifaa vya kutosha, lakini sasa tuna matumaini kuwa maktaba hii itasaidia kuongeza kiwango cha elimu na kuhamasisha wanafunzi kujituma zaidi,” alisema mmoja wa walimu. Wananchi wa Lendikinya walikubaliana na walimu, wakiwa na matumaini makubwa ya kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi. “Tunaamini kuwa elimu itabadilika kwa kiwango kikubwa kwa sababu ya maktaba hii. Tunashukuru kwa msaada huu na tunatarajia watoto wetu kufikia malengo yao,” aliongeza mmoja wa wananchi. Maktaba hii ya kisasa inajumuisha vitabu mbalimbali, vifaa vya kujifunzia, na maeneo ya kisasa ya kujisomea. Kwa sasa, itakuwa ni alama ya maendeleo ya elimu katika wilaya ya Monduli na ni mfano wa juhudi za jamii na mashirika ya kiraia kusaidia kukuza elimu nchini.