У нас вы можете посмотреть бесплатно RC LINDI AKABIDHI MAGARI KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LINDI, ATOA KAULI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, Leo Oktoba 24, 2025, amekabidhi vitendea kazi kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Lindi, wakati wa zoezi la utayari uliohusisha na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Lindi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuimarisha utendaji na kukabiliana na changamoto wakati wa utendaji na utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Vitendea kazi vilivyokabidhiwa leo ni Magari ya ufuatiliaji na usimamizi pamoja na gari la wagonjwa la kisasa, Coman Car, Mtambo (Motor) Unaobeba Litre 5,000 za maji na povu la kemikali (chemical foam) ujazo wa lita 400 pamoja na gari dogo la ukaguzi. Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Telack alisema Serikali imeendelea kuwekeza katika kuwajengea uwezo vyombo vya Ulinzi na Usalama ili viweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi na kutoa huduma bora kwa wananchi. Aidha, aliwataka maafisa wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuimarika hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025. Kwa upande wake, Mrakibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Lindi, Joseph Mwasabeja ameishukuru Serikali kwa kuleta vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto zilizokuwa zinajitokea wakati wa utekelezaji wa majukumu yao. Follow Us Istagram @mashujaaradio Facebook #mashujaafm Youtube #mashujaatv