У нас вы можете посмотреть бесплатно Mhe Dkt Doto Mashaka Biteko akitoa salamu za Serikali kwenye mazishi ya Askofu Chediel Sendoro или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na viongozi wa dini ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao ya kitume kwa maendeleo ya Watanzania. Dkt. Biteko amesema hayo leo Septemba 17, 2024 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mwanga, Kanisa Kuu lililopo Mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya ibada ya mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, Chediel Sendoro. Askofu Sendoro amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Septemba 9, 2024 katika eneo la Kisangiro wilayani Mwanga. "Rais yupo tayari kushirikiana na kanisa wakati wowote ili kanisa liweze kufanya kazi zote za kitume na sisi tuko tayari kuifanya Tanzania iwe bora na Watanzania waishi vizuri katika nchi yao," amesema Dkt. Biteko. Ameongeza kuwa msingi wa Dayosisi hiyo umejengwa kwa upendo na kuwa moja ya kazi kwa viongozi wa kanisa hilo ni kupata mtu atakayeendeleza kazi na maono ya Askofu Sendoro juu ya kanisa hilo. Amefafanua kuwa kila binaadamu ataiaga dunia itakapofika wakati wake ispokuwa kila mmoja aliyehai amefanya nini na hivyo hawana budi kukumbuka mahubiri ya Askofu Sendoro na umoja alioujenga miongoni mwao. "Natoa pole kwa familia, wazazi, mjane, watoto na wajukuu kwa kuwa Septemba 9, 2024 lilitokea jambo lisilo la kawaida na kuondokewa na Askofu Sendoro. Nakupa pole Askofu Mkuu wa Kanisa, maaskofu wote na Wanamwanga, tuyaenzi yote aliyokuwa akiyaishi, alijali sana maadili yetu naomba tena tuendelee kuliombea Taifa na nchi yetu." Amesisitiza Dkt. Biteko.