У нас вы можете посмотреть бесплатно GADI SEDEKIA MDOGO WAKE NA MUIMBAJI FANUEL SEDEKIA ANAHITAJI MSAADA WETU ILI APATE MATIBABU YA FIGO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mdogo wa aliyekuwa mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili Tanzania, FANUEL SEDEKIA, anaye fahamika kama Gadi Sedekia, amekuwa kwenye mapambano makubwa ya kiafya kwa takribani miaka 16, akipambana na changamoto ya kisukari tangu akiwa na umri wa miaka 19 tu. Miaka iliposogea, ugonjwa ulianza kuathiri mwili wake zaidi, na hatimaye figo zake zikafeli na kusababisha hali ngumu ya afya iliyomsukuma kuingia kwenye matibabu ya Dialysis kwa zaidi ya miaka miwili (2) sasa. Kila wiki Gadi hulazimika kwenda hospitali kupimwa na kufanyiwa dialysis ambayo humgharimu takribani Shilingi 600,000/= kwa wiki — gharama ambayo si kila mtu anaweza kuivumilia. Lakini pamoja na yote haya, bado yupo mtu aliyejitokeza na moyo wa huruma — msamaria mwema aliyekubali kutoa figo moja ili Gadi apate nafasi mpya ya maisha. Hata hivyo, safari ya upandikizaji wa figo bado imekwama kutokana na gharama kubwa ya upasuaji ambayo inafikia takribani Shilingi Milioni 50/=, fedha ambazo Gadi hawezi kuzifikia mwenyewe. Leo, anatoa wito kwa Watanzania, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Kidini, Viongozi wa Deni, Waimbaji wa Nyimbo za Injili na Watumishi wa Mungu, Mashirika, Taasisi za Afya na Wadau wa Kijamii Kumsimamia kijana huyu, ambaye si tu amepoteza afya yake kwa miaka mingi, bali pia matumaini yake yanategemea msaada wa jamii yake. Tuonyeshe upendo kama taifa, tuoneshe huruma kama binadamu, na tuoneshe mshikamano kama ndugu. Kila mchango — mkubwa au mdogo — unaleta pumzi mpya ya matumaini. Namba ya mchango (M-Pesa): NMB BANK ACC/NO. 42510005391 MAJINA: GADI KAPARARE SEDEKIA M-PESA +255765113586 MAJINA: GADI SEDEKIA Kwa Gadi, changamoto hizi hazina majibu ya kibinafsi — ndio maana leo anakuja kwa Watanzania. Tuwe sehemu ya kumrudishia afya, heshima na maisha, ikiwa bado anayo ndoto ya kutimiza yeye kama Kijana wa Kitanzania