У нас вы можете посмотреть бесплатно RAIS WA FEMATA AFANYA KIKAO NA WACHIMBAJI – Karimjee Hall или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Rais wa FEMATA Mhe John Wambura Bina leo kikao maalum na wachimbaji wa madini wanaotarajia kusafiri kwenda Canada, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Hall jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika kikao hicho, Rais wa FEMATA aliwataka wachimbaji hao kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania kwa kuzingatia nidhamu, weledi na uzalendo wanapokwenda nje ya nchi. Alisisitiza kuwa safari hiyo ni hatua muhimu katika kukuza ujuzi, kubadilishana uzoefu na kujenga ushirikiano wa kimataifa utakaoimarisha sekta ya madini nchini. Aidha, alieleza kuwa kupitia ziara hiyo, wachimbaji watapata fursa ya kujifunza teknolojia za kisasa za uchimbaji, usimamizi bora wa migodi pamoja na mbinu za kuongeza thamani ya madini kabla ya kuuzwa nje ya nchi. Kwa upande wao, wachimbaji walionesha shukrani kwa uongozi wa FEMATA kwa kuwawezesha kushiriki safari hiyo, wakiahidi kurejea na maarifa na uzoefu utakaochangia maendeleo ya sekta ya madini na uchumi wa taifa kwa ujumla.