У нас вы можете посмотреть бесплатно Mathayo l6:13-19 | Injili ya Jumapili ya wito wa mt Petro na Paulo | Mwaka C 29/6/2025 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mathayo l6:13-19 Nitakupa wewe Petro, funguo za uzimani. 1.Kufika Kaisaria, Yesu liwaulizia. Swali akitamkia, wanafunzi kujibia. "Nani wanifikiria, vipi watu wanitia. Ndo wao wakajibia, heshima kitamkia. Nitakupa wewe Petro, funguo za uzimani. 2.Wengine wanasemea, Yohana mbatizaji. Ni Eliya wamwonea, nabii aliyetaji. Wengine ni Yeremia, mwinjilisti msemaji. Mmoja lotabiria, pale kale kwa vijiji. Nitakupa wewe Petro, funguo za uzimani. 3.Yesu kawageukia, swali lake kutamka. "Ninyi mnanisemea, mimi ni nani hakika?" Kimya kikatawalia, hewa ikatetemeka. Simoni kasimamia, moyo wake ukiwaka. Nitakupa wewe Petro, funguo za uzimani. 4.Kwa uthabiti kasema, kwa sauti ya imani. "Wewe ndiwe Kristo mwema, Mwana wa Mungu Mbinguni." Kafurahi Yesu mwema, kusikia ya Simoni. Yale aliyoyasema, ni heri kwake Manani. Nitakupa wewe Petro, funguo za uzimani. 5."Petro heri umejawa, wewe mwana wake Yona. Si mwili damu kupewa, kujuwa uliyonena. Ni Baba alifunuwa, hayo yote ulonena. Wewe ni mwamba takuwa, Kanisa langu kufana. Nitakupa wewe Petro, funguo za uzimani. 6."Jehanamu milangoni, halitakushinda kamwe. Funguo za ufalmeni, nikakukabidhi wewe. Ufungacho duniani, mbinguni pia kifungwe. Na ulichofunguani, na huko kifunguliwe. Nitakupa wewe Petro, funguo za uzimani." Na Malenga Ibura Bokeny Ochigo 26/6/2025