У нас вы можете посмотреть бесплатно WANANCHI WA BUMBULI BEGA KWA BEGA NA MAKAMBA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mbunge wa Bumbuli na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), January Makamba amesema yeye na wananchi wa jimbo hilo wana mengi ya kujivunia kwani, wamepita milima na mabonde kwenye harakati za kusaka maendeleo. Amesema maendeleo makubwa yaliyopatikana kwenye jimbo hilo kwa sasa, hayawezi kulinganishwa na miaka iliyopita na kwamba, safari bado inaendelea. Makamba, ambaye amepata kuhudumu kwenye wizara mbalimbali ikiwemo Nishati na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ameyasema hayo wakati wa mikutano mbalimbali jimboni humo. Katika mkutano ya ziara zake hizo, Makamba amewaomba wananchi wake kuendelea kujenga Imani kwa Rais Samia Suluhu Hassan na CCM kwani, wana dhamira ya dhati ya kuendelea kuwaletea Watanzania maendeleo ya haraka. Kwa mujibu wa Makamba katika baadhi ya sekta kama afya, kwa sasa zahanati kwenye jimbo hilo zimefikia 39 kutoka 14 huku upatikanaji wa majisafi na salama ukifikia asilimia 78 kutoka asilimia 37. Kwa sasa Makamba ameeleza wananchi kuwa barabara ya Soni-Bumbuli hadi Korogwe itajengwa kwa kiwango cha lami na tayari Rais Samia amesema mchakato wake umeanza ikiwemo kutangazwa kwa zabuni ili kumpata mkandarasi.