У нас вы можете посмотреть бесплатно Kipindi cha Ujuzi ni Maisha Mafunzo kwa madereva wa magari makubwa или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Takwimu mbalimbali zinaonyesha kuwa ajali nyingi za barabarani katika ukanda wa Afrika Mashariki zinatokana na kutozingatia sheria za barabarani na hilo huchangiwa kwa kiasi kikubwa na madereva wengi kuendesha magari pasipo kupitia mafunzo stahiki. Tanzania imetunga sheria na taratibu nzuri za vyombo vya usafirishaji na matumizi ya barabara. Miongoni mwa sheria na taratibu hizo ni pamoja udhibiti wa mwendo kasi, kuzuia mtu kuendesha akiwa amelewa na kuhimiza matumizi ya vifaa vya usalama kama mikanda, kofia za ngumu yaani Helmet na hata viti maalumu kwa watoto. Hata hivyo, madereva wengi hawazingatii. VETA inatambua changamoto hiyo na imekuwa ikihimiza mafunzo kwa watumiaji wote wa vyombo vya moto na imekuwa ikitoa mafunzo ya udereva karibu katika kila chuo chake. Katika kipindi hiki tumeangazia Mchango wa VETA juu ya Mafunzo kwa madereva wa magari makubwa yanayotolewa katika chuo cha VETA Kihonda mkoani morogoro.