У нас вы можете посмотреть бесплатно KAMBI YA MADAKTARI BINGWA YALETA TUMAINI JIPYA KWA WANASINGIDA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, amezindua rasmi kambi ya uchunguzi na matibabu inayotolewa na Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH). Uzinduzi huo umefanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, ukiashiria hatua mpya ya kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi. Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Dendego amepongeza uwekezaji unaoendelea kufanywa na Serikali katika sekta ya afya, akibainisha kuwa maboresho hayo yametokana na dhamira ya uongozi wa kitaifa ya kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi kwa wakati. Amesema programu za huduma mkoba ni mkakati mahsusi wa kupanua wigo wa matibabu ya kibingwa katika maeneo yenye uhitaji mkubwa. Katika salamu zake, ameupongeza uongozi wa BMH kwa kuleta timu ya wataalamu pamoja na magari maalumu yenye vyumba vya upasuaji, akieleza kuwa hatua hiyo inaonesha uwajibikaji na weledi wa taasisi za umma katika kuboresha afya ya wananchi. Amesisitiza kuwa uwepo wa huduma hizo mkoani Singida ni fursa muhimu kwa wananchi kupata matibabu ya kibingwa kwa gharama nafuu na kwa ukaribu zaidi, badala ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma nje ya Mkoa. Amewahimiza wakazi wa Singida na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kunufaika na huduma hizo. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Bw. Suleimani Mwenda, amesema kambi hiyo ni hatua ya kimkakati katika kuimarisha huduma za afya wilayani humo. Ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, sekta ya afya imeimarika kwa kasi kupitia ongezeko la watumishi, ujenzi wa zahanati 13 na vituo vya afya saba, pamoja na maboresho ya miundombinu ya tiba na huduma kwa wagonjwa. Amesema hatua hizo zimeongeza uwezo wa utoaji huduma na kupunguza changamoto za upatikanaji wa matibabu hususan kwa wananchi wa maeneo ya vijijini. Mapema, akizungumza kwa niaba ya BMH, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo na Huduma Mkoba, Dkt. Emiliana Biovera, amesema hospitali hiyo sasa inatoa zaidi ya huduma 20 za kibingwa na huduma 18 za ubingwa bobezi. Ameeleza kuwa upanuzi huo wa huduma umechangia kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda Dar es Salaam na hata nje ya nchi. Miongoni mwa huduma zinazotolewa ni upandikizaji figo, upandikizaji uloto, huduma za radiolojia, upasuaji kwa njia ya matundu madogo (laparoscopic surgery), upandikizaji wa nyonga na magoti, upasuaji wa moyo na mishipa ya damu pamoja na matibabu ya mawe kwenye figo na njia ya mkojo. Akitoa salamu za Katibu Tawala wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Victorina Ludovic, ameishukuru Serikali na uongozi wa Mkoa kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya afya. Amesema uwepo wa kambi hiyo ni faraja kubwa kwa wananchi wa Singida kwani unawapa fursa ya kupata huduma za kibingwa karibu na makazi yao, huku ukisaidia kupunguza mzigo wa rufaa na kuimarisha kinga na tiba mapema. Kambi hiyo inatarajiwa kuhudumia mamia ya wananchi wa Singida na maeneo ya jirani, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya za kibingwa kwa usawa na ufanisi zaidi.