У нас вы можете посмотреть бесплатно VIONGOZI WA M23 WAKUTANA NA WAKUU WA MAJESHI SADC, WAKUBALIANA HAYA… или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Goma. Wakuu wa Majeshi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na uongozi wa wapiganaji wa kundi ka M23 wamekubaliana kupunguza mvutano ili kuwezesha suluhisho la amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Katika mkutano uliofanyika Mjini Goma jana Ijumaa Machi 28, 2025, pande zote ziliahidi kuheshimu usitishaji mapigano na kuondoka kwa vikosi vya SAMIDRC bila masharti yoyote. Wakati wa mazungumzo, pande husika zilifikia makubaliano ya kuruhusu kuondolewa haraka askari wa Kikosi cha walinda amani wa SADC nchini DRC la SAMIDRC, silaha na vifaa vya kijeshi huku wakiacha mali nyingine za kijeshi za FARDC. “Timu ya AFC/M23 itaratibu uhuru wa harakati za SAMIDRC kwa ajili ya maandalizi ya kuondoka kwao kulingana na kanuni zilizokubaliwa,” ilisema sehemu ya taarifa ya pamoja ya pande hizo. Zaidi ya hayo, walikubaliana kuhakikisha kuwa M23 inaratibu shughuli ya kuondoka kwa askari wa vikosi vya SAMIDRC kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa. M23 na SADC pia walikubaliana kufanya tathmini ya pamoja ya kiufundi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Goma ili kutathmini hali yake ya kufunguliwa tena. Aidha, pande hizo zilifikia makubaliano ya kufanya mkutano wa ufuatiliaji katika tarehe na mahali yatakayokubaliwa ili kutathmini maendeleo ya ahadi zilizowekwa. Imeandikwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa Mashirika.