У нас вы можете посмотреть бесплатно WANANCHI WAANDAMANA DAR "MWAKILISHI WA RAIS ANAKESI NA SISI TUSIPEPESE MACHO HAPA" или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mzozo umeibuka kati ya baadhi ya wananchi wa eneo la Buza Kanisani katika wilaya ya Temeke na Mkuu wa Wilaya hiyo, Sixtus Mapunda, kufuatia uamuzi wa kusitishwa kwa ruti ya daladala zilizokuwa zikifika Buza Kanisani. Wananchi hao wamelalamikia hatua ya kuyafanya magari hayo kuishia katika stendi mpya ya Kwa Mama Kibonge badala ya kufika Buza Kanisani kama ilivyokuwa awali. Wamesema mabadiliko hayo yameongeza umbali wa kutembea kwa abiria pamoja na gharama za usafiri kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, amesema uamuzi huo umefanywa kwa lengo la kuboresha mpangilio wa usafiri na kupunguza msongamano katika maeneo ya barabara. Amesisitiza kuwa mamlaka zinaendelea kusikiliza maoni ya wananchi ili kupata suluhisho litakalowafaa pande zote. Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa Buza Kanisani wameitaka serikali ya wilaya kutathmini upya uamuzi huo ili kuruhusu daladala kurejea kwenye ruti ya awali, wakidai hatua hiyo itarahisisha huduma ya usafiri kwa wakazi wengi wa eneo hilo.