У нас вы можете посмотреть бесплатно KILIMO BIASHARA / MALKIA WA KILIMO BIASHARA MWANZA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Undani wa leo unamwangazia malkia wa nguvu kutoka Mkoani Mwanza Joyce Kabago mwalimu wa shule ya sekondari Lebuka na Mkurugenzi wa Lake Zone Farm ambaye ni mshindi wa tuzo ya Malkia wa nguvu katika kipengele cha kilimo biashara. Nini kimempa upekee wa tuzo hiyo kutoka kanda ya ziwa? Hapa tunaungana na Thuwaiba Jamal ambaye anatupitisha kwa ufupi kwenye Makala hii ya Undani wa leo. Kutoka Kanda ya ziwa Rock City Mwanza Jukwaa la Malkia wa Nguvu 2025 linakukutanisha na Malkia wa nguvu Joyce Kabago Mwalimu wa shule ya sekondari na Mkurugenzi wa Lake Zone Farm, shamba kubwa la mifugo aliyeacha kuishi na mifugo na kufuga. Na si kufuga tu, Joyce anafuga kidigiti kwa kubuni na kutumia teknolojia za kisasa kiasi cha kuongeza uzalishaji na kurudufu kipato kwa kupunguza gharama za uendeshaji. Marafiki na watu wa karibu na Joyce waliupiga mwingi mno walipomshauri kukopa na kuboresha miundombinu ya ufugaji lakini tui likaingia maji, almanusura Joyce atoke mchezoni. Nakukumbusheni tena Joyce haishi na mifugo bali ni mfugaji kwani humu ndani ukihitaji mayai utapata kontena na ukihitaji mbegu bora ya nguruwe utapata zizi zima. Safari ya mafanikio haijawahi kunyooka mithiri ya rula bali huja na muundo wa kingo za mto, Joyce hatosahau wakati ambao akiwa na mkopo mkubwa banki, na kuku wake karibu woote walikufa ilibaki ivii tu Joyce aokote makopo kwa stress. Malkia wa Nguvu 2025 linamtambua Joyce kama shujaa wa kilimo biashara, basi ndugu zangu Waluo na Wakurya wa kanda maalumu namleta mtani wenu Joyce Kabago mpokeeni kwa shangwe.