У нас вы можете посмотреть бесплатно DAS Mbeya: Kipato Kisiharibu Vyanzo vya Maji или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya, Bw. Azizi Faki, ametoa onyo kali juu ya kuendelea kwa uharibifu wa vyanzo vya maji wilayani humo, akisema hali halisi ya uchafuzi na upungufu wa maji inaonekana wazi kutokana na shughuli za kibinadamu zisizozingatia sheria. Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa chanzo cha maji cha Mtombalizi, kilichopo katika Kata za Utengule Usongwe na Nsalala, Bw. Faki alisema uchimbaji wa mchanga na mawe katikati ya mto pamoja na uharibifu wa kingo za maji umepelekea mto huo kupoteza mwelekeo wake wa asili, maji kuchafuka na kupungua kwa kiasi kikubwa. Bw. Faki alisema licha ya kuwepo kwa maelekezo ya awali ya kulinda kingo za mito, kupanda miti na kuacha mita sitini kutoka kwenye chanzo cha maji bila shughuli za kibinadamu, hali bado ni mbaya kutokana na kuendelea kwa shughuli haramu, hali inayohatarisha vyanzo vya maji vinavyotegemewa na wananchi wa sasa na vizazi vijavyo. Alitoa wito kwa taasisi zote husika ikiwemo TFS, mamlaka za maji, mamlaka ya madini, Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa, pamoja na viongozi wa serikali za mitaa, kata na tarafa kushirikiana kikamilifu katika kulinda chanzo hicho. Alisisitiza kuwa jitihada za kutafuta kipato haziwezi kuwa sababu ya kuvunja sheria na kuharibu mazingira.