У нас вы можете посмотреть бесплатно Bandari: Ugomvi wa ubinafsishaji или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Ubinafsishaji wa bandari au uendeshaji wa baadhi ya maeneo ya bandari umekuwa ni mfumo uliopata umaarufu hivi karibuni. Mifumo hii sasa imefikia katika pwani za Afrika. Licha ya nchi nyingi za Afrika kuwa na miundombinu ya bandari, lakini uendeshaji na ufanisi wa bandari hizo umekuwa tatizo. Hii ikichangiwa na ukosefu wa vifaa vya kisasa licha ya kuwa na faida ya kijiografia. Afrika pia imebarikiwa na mali ghafi tele… Ni kutokana na hali hiyo, ndio imekuwa kichocheo kikubwa kwa nchi na mashirika yenye nyenzo na uzoefu mkubwa wa kuendesha bandari kama UAE, Singapore, Uholanzi na China imefanya iwe rahisi kwa waendeshaji wa kigeni kupata mikataba katika nchi ambazo zinatatizikia kuendesha na kuendeleza bandari zao. Nchi za Kiafrika pia zinafungua milango kwa uwekezaji wa ubinafsishaji ambao utanufaisha wawekezaji na wamiliki. Bandari zilizopo katika eneo la Bahari ya Hindi na Bahari Nyekundu ni njia kuu za biashara na mnyororo wa usambazaji wa kimataifa. Zipo katika njia za usambazaji wa mafuta na gesi na kwenye sehemu ya mpango ya njia mpya za biashara inayo buniwa na China inayojulikana kama “Belt & Road.” UAE kupitia shirikia la DP World (Dubai Ports World) ni muwekezaji mkubwa wa bandari Afrika baada ya China, Ulaya na Marekani. Bandari za kisasa zinahitaji uwezo wa kufikia uchumi wa hali ya juu (economies of scale) na kuhudumia meli zenye makontena makubwa ambazo zinaathiri sana biashara ya kimataifa. Kimsingi, huwezi kuwa kitovu kikuu cha biashara na vifaa bila miundombinu na uendeshaji wa bandari kubwa. Hapa ndipo ubinafsishaji unapojitokeza. Fuatilia Habari zetu: 🌐 https://www.trtafrika.com/sw Tiktok 🟣 / trtafrikasw Facebook 🔵 / trtafrikasw Youtube 🔴 / @trtafrikasw X ⚫ https://x.com/trtafrikaSW Instagram 🟣 / trtafrikasw