У нас вы можете посмотреть бесплатно NEWALA DC YAGAWA MICHE 92,000 YA MIKOROSHO KUONGEZA UZALISHAJI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Halmashauri ya Wilaya ya Newala (Newala DC) imezalisha miche 92,000 ya mikorosho kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hilo linalochangia kwa kiasi kikubwa kipato cha wananchi na mapato ya Halmashauri. Mratibu wa ugawaji wa miche Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Bi. Maria Peter, amesema miche hiyo itagawiwa kwa wananchi katika tarafa zote nne za Mchemo, Mkwedu, Kitangari na Chilangala, ambapo kila tarafa itapatiwa miche 23,000. Amesema hatua hiyo inalenga kuongeza uzalishaji wa korosho kutoka tani 25,000 zilizovunwa mwaka uliopita hadi kufikia tani 30,000 hadi 40,000 ndani ya miaka mitano ijayo. Baadhi ya wakulima walionufaika na mgao huo, akiwemo Ndugu Juma Hasani Mkauja na kijana Juma Abdala Matulia, wameishukuru Serikali kwa mpango huo, wakisema unawapa matumaini ya kuongeza uzalishaji na kipato kupitia zao la korosho. Uzalishaji wa miche hiyo ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Bodi ya Korosho Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri na vyama vikuu katika mikoa inayolima korosho, wenye lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hilo nchini kutoka tani laki 7 hadi kufikia tani milioni moja ifikapo mwaka 2030.