У нас вы можете посмотреть бесплатно CHEKECHE | Kuna maana gani kwa nchi ya Palestina kutambuliwa? или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umegeuka kitovu cha mijadala ya kidiplomasia duniani, ambapo hoja kubwa imekuwa juu ya kutambuliwa kwa taifa la Palestina. Wakati Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alipoinuka kuhutubia, kundi kubwa la wajumbe lilitoka ukumbini kama ishara ya upinzani. Mataifa mengi ya Ulaya yameendelea kupigia chapuo ajenda ya Palestina, yakionyesha mshikamano na watu wa Gaza walioko katikati ya machafuko. Hata hivyo, Marekani imeendelea kusimama upande wa Israel, ikipuuzia shinikizo la jumuiya ya kimataifa na kilio cha maafa yanayoripotiwa kila siku. Kutokuwepo kwa kauli ya pamoja kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa kunatoa picha ya dunia iliyogawanyika, huku swali kubwa likibaki, hatua hii ya kutambuliwa kwa Palestina itasababisha mabadiliko ya kweli ya kisiasa, au itaishia kuwa alama nyingine ya mgawanyiko wa kimataifa? #AzamTVUpdates Mhariri | John Mbalamwezi