У нас вы можете посмотреть бесплатно MAALIM SEIF AKUMBUKWA MIAKA MITANO IMETIMU LEO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Chama cha ACT-Wazalendo kimeadhimisha miaka mitano tangu kufariki kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Seif Sharif Hamad, kwa dua maalum zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo Msikiti wa Barza. Dua hiyo iliofanyika Masiji hiyo iliopo Mchambawima eneo la Mji Mkongwe Zanzibar ilihudhuriwa na viongozi wa kitaifa wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa sasa, Othman Masoud Othman, Makamu Mwenyekiti wake Zanzibar Ismail Jussa pamoja na Mwenyekiti mstaafu Juma Duni haji. Akizungumza wakati wa dua hizo, Hassan Jan Masoud, ambaye aliishi na kufanya kazi kwa karibu na Maalim Seif wakati wa uhai wake, alieleza sifa mbalimbali za kiongozi huyo. Alisema Maalim Seif alijitahidi kuondoa ubaguzi na kuimarisha umoja miongoni mwa Wazanzibari. Aidha, alibainisha kuwa Maalim Seif alipigania kuasisiwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ili kuhakikisha Wazanzibari wanakuwa kitu kimoja na kuishi kwa mshikamano. Aliongeza kuwa kiongozi huyo ni mfano wa kuigwa, na waliobaki wana wajibu wa kuyaendeleza mema yote aliyoyaacha. Maalim Seif alifariki dunia tarehe 17 Februari 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, akiwa bado anahudumu kama Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika siasa za vyama vingi nchini Tanzania na kimataifa. Kwa upande wake, Nassor Ahmed Mazrui aliwashukuru wanachama na wananchi kwa ujumla kwa kuendelea kumuenzi kiongozi huyo kupitia dua na matendo mema.h