У нас вы можете посмотреть бесплатно KAMATI YA SIASA TUNDURU YAKAGUA MRADI WA SKIMU KUBWA YA UMWAGILIAJI NAMBARAPI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Tunduru imeendelea na ziara yake kwa siku mbili mfululizo, ambapo leo tarehe 24 Februari 2026 imetembelea na kukagua maendeleo ya Mradi wa Skimu Kubwa ya Umwagiliaji Nambarapi uliopo Kata ya Masonya, Wilaya ya Tunduru. Mradi huo unasimamiwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Unatekelezwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 6.3, ukiwa na lengo la kuboresha sekta ya kilimo na kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo. Kazi zinazoendelea katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa banio na tuta, mfereji mkuu, mifereji ya upili, mfereji wa matupio, barabara za mashambani, vivusha maji pamoja na ujenzi wa ofisi ya mhandisi. Hadi sasa, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 36. Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tunduru, Abdallah Mtila, alisema mradi huo ni ushahidi wa dhamira ya Serikali ya kuwekeza katika sekta ya kilimo na kuboresha maisha ya wananchi. “Mradi huu ukikamilika hautakuwa wa msimu, bali utawezesha uzalishaji wa kilimo kwa mwaka mzima. Kuimarika kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja ndiko kunakoimarisha uchumi wa taifa kwa ujumla. Halmashauri ya Wilaya inapaswa kushirikiana kwa karibu na Tume ya Umwagiliaji ili kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati,” alisisitiza Mtila. Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe.Denis Masanja, alieleza kuwa licha ya kuchelewa kukamilika kwa wakati, bado kuna umuhimu wa kuongeza jitihada katika usimamizi wa mradi huo. Alibainisha kuwa mradi huo ni fursa muhimu ya kuongeza uzalishaji wa kilimo, kukuza kipato cha wakulima na kukabiliana na changamoto za ukame zinazoathiri wakulima wa eneo hilo. Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji Nambarapi ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuendeleza sekta ya kilimo nchini na kutatua changamoto za ukame katika maeneo mbalimbali. Kukamilika kwake kunatarajiwa kuwa mfano wa mafanikio kwa maeneo mengine yenye changamoto zinazofanana.