У нас вы можете посмотреть бесплатно DONDOO:Shetani ni wewe mwenyewe!. Nguu za Jadi UK 115..Ukweli wa kauli IBILISI WA MTU NI MTU или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
"Ndugu zangu. Kwanza ninawaomba msamaha Kwa maovu yote ambayo niliwatendea. Nimlaani shetani..." "Shetani ni wewe mwenyewe! Shetani wa mtu ni mtu!" 1. Tambua muktadha wa dondoo hili Al. 4 2. Tetea kauli kuwa shetani wa mtu ni mtu Ukirejelea riwaya ya Nguu za Jadi Al.16 UK 115 MTINDO 1. Hotuba- Mrima kuanza usemi Kwa neno ndugu zangu .. 2. Nahau: omba msamaha (kutaka Rashi), laani shetani (kemea mwovu) 3. Mdokezo: Ninamlaani shetani... 4. Kisengere nyuma: Maovu yote niliyowatendea 5. Nidaa: Shetani ni wewe mwenyewe! 6. Methali: Shetani wa mtu ni mtu 7. Dayolojia 8. Litifati- Ninaomba msamaha ni matini yaliyonukuliwa kutoka Biblia Takatifu IBILISI WA MTU NI MTU Ibilisi sasa shetani (malaika mkuu aliye hasi sheria za Mungu hivyo anaaminika kuwa mwovu). Methali ibilisi wa mtu ni mtu inamaanisha kuwa adui wa binadamu ni binadamu mwenziwe haswa wa karibu kwani atamwendea kinyume au atakuwa mshawishi wa maovu. 1. Chifu Mshabaha kuwazunguka Waketwa Kwa kushiriki Kwa kuchomwa Kwa makazi yao. 2. Nanzia kuwa karimu kwa Wanamatango Kwa kuleta msaada wa chakula hasa Cha watoto ilhali hakuwatembelea watu walio na shida wala kuwajali maskini. Kusudi lilikuwa kuwafumba watu macho. 3. Sagilu kumpa Mrima pesa za kulewa kisha kumdhihaki mbele ya Mangwasha eti ni kijana mlevi 4.Chifu Mshabaha kumlazimisha Mangwasha kukubali usuhuba wa Sagilu ilhali alikuwa mwajiri wa Mangwasha. 5. Sagilu kumla mwanawe kivuli Kwa kufanya usinzi na Cheiya (mchumba wa Mashauri) 6.Sihaba kutumwa na Sagilu kulipiza kisasi kwa kuchukua kifurushi kilicholipuka siku ya harusi baina ya Mrima na Mangwasha 7.Sagilu kuwa na usuhuba na Nanzia ambaye ni mke wa rafikiye (Mtemi Lesulia) aliyempa kazi ya ku 8. Cheiya kutumwa na Mtemi Lesulia kumtilia Lonare sumu kwenye kinywaji ili kumwangamiza 9. Mwanasheria Mafamba kuficha majalada na nyaraka muhimu zilizohusu kesi za ufisadi uliokithiri katika jamii hivyo kuendeleza maovu. 10. Sihaba kufungua jumba la RBL lililotumiwa kwa ukahaba hivyo kudunisha hadhi ya vigoli na pia kudorora Kwa maadili. 11. Kina mama kuchuuza binti zao wachanga ili wapate hela 12. Ngoswe kushiriki biashara ya mihadarati iliyodhuru watu haswa vijana wa shule. 13. Mashauri kushirikiana na babake kufisidi nchi vipusa na hata kuangusha majumba 14. Wakule kuwachukia Waketwa kiasi Cha kuwanyima nafasi za ajira. 15. Mtemi Lesulia na Sagilu kutumia hongo ili kuvuruga kampeni na hata kura za wapinzani wao 16. Mrima kuchezesha Mangwasha kayamba Kwa kuwa na kiruka njia, kutelekeza familia yake na hata kutowajibika. 17. Mrima kuwatendea Waketwa kinyume Kwa kuharibu na anapofunga njia za Mwamba ndipo mpinzani wake ashinde kura UK 110 18. Mangwasha kuwaza jinsi watu walivyokuwa mahasidi wa kuangamiza wenzao. Waovu waliootea kwenye vichochoro, vijia faragha za kila njia. Mabedui waliozoea vya kunyonga lakini vya kuchinja hawaviwezi. Kwa kutumia hila au hela, wakawawekea wengine mitego hatari ili waangamie. Mashukio yao yawe ya kuchukiza vizazi na vizazi 19. Polisi kumwachilia Sihaba licha ya makosa ya Jinai aliyotenda hivyo kukosesha waliodhulumiwa kutopata haki yao. 20. Sagura anadokeza kuwa dunia yote inajua aliyemsaliti Yesu Kristu. Yuda alikuwa mwanafunzi wa Yesu kisha akamsaliti hivyo -kuthibitisha ukweli wa methali "IBILISI WA MTU NI MTU." 21. Sagilu na aila yake kuwakunjia Waketwa ngumi kwa kuwapangia maovuUK 114 22. Mbwashu kufisidi Pato la nchi na kupelekea mfumuko wa bei 23. Chifu Mshabaha kumpiga Mangwasha kalamu licha ya huduma aliyotoa. 24. Sagilu kuagiza bidhaa ghushi zinazodhuru afya ya umma k.v maziwa ya watoto yenye sumu 25. Wakwasi kuwatesa wachochole haswa kubadilisha mikondo ya maji kuelekea mashamba yao hivyo kuhangaisha wananchi waliotegemea mito na Vijito hivyo. 26.. Lesulia kutawala Kwa mkono wa chuma Kwa kutumia sera za ubaguzi hivyo kuchangia kudorora Kwa huduma, ajali na vifo. 27. Sagilu kuwanyemelea wake za watu 28.. Wapinzani wa Lonare kumteka nyara na kumnyanyasa kiasi Cha kumdhuru 29. Sihaba na Sagilu kumshawishi Mbaji kuacha kazi ya Lonare 30. Biashara za Lonare kuwa na changamoto kutokana na hila za wapinzani wake. 31. Kuhangaisha kupata leseni ya biashara 32. Kunyanganywa leseni Kwa Mafamba na hakimu baada ya Waketwa kushinda kesi ya ardhi dhidi ya serikali.