У нас вы можете посмотреть бесплатно NIWAJIBU WETU KUWATEGEMEZA WACHUNGAJI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
IBADA YA JUMAPILI 11 DECEMBER 2022 ANDIKO: Hesabu 18:8-15, 20 - 21. Kati ya makabila 12 ya Israel, walawi ndio waliopewa urithi wa madhabahuni. Makabila mengine walipewa urithi wa duniani. Matoleo yao katika masinagogi ilikuwa ni mali ya makuhani. Kutoa kwetu ni kuwategemeza watumishi wa Mungu. Ni wajibu kuwategemeza kwa vitu (material) na maombi. KATIKA AGANO LA KALE Hesabu 18:20 Mungu alielekeza moja kwa moja walawi kunufaika na vile vyote vya madhabahuni. Haruni na Lawi hawakuwa na kitu cha kurithi isipokuwa Bwana mwenyewe. Kuwategemeza ni mkumtanguliza Mungu kwetu na ni wajibu kwetu. Kumb 18:1-5 Watumishi tunaowategemeza ni watu ambao wameitwa na Mungu, wanatangulia baadala yetu, na kuwajibika kwetu. Kuwategemeza ni wajibu wetu, ni wajibu wa kanisa, ni kumtii Mungu. KATIKA AGANO JIPYA. Matendo 12:1-17 Kama ilivyo katika agano la kale linafundisha kutegemeza na katika agano jipya linafundisha hivyo pia. Kuna kutegemeza kwa vitu na kwa maombi kama nilivyosema mwanzo. Kupitia maombi kanisa lilimtegemeza Petro, maombi yako yana dhamani kubwa, waliomba kwa bidii, ajenda yao ilikuwa kumwombea Petro. Wanahitaji faraja na kutiwa moyo kutoka kwetu. Wajibu wa kuwaombea ni wetu, kanisa la kwanza waliwajibika juu ya Petro, na baada ya kutoka gerezani aliwakuta wanaomba. WAFILIPI 4:14- 20 Filipi ni kanisa lililosimama na mtume Paulo, Hata hapa SRC mchungaji akianza na mshirika mmoja, leo tunaabudu katika kanisa zuri, ina maana kuna watu walimtegemeza mchungaji kwa maombi yao. Kanisa liliingia ubia na Paulo lakini bado walimtegemeza kimwili pia. Musa alitegemezwa kwa kushikwa mikono, Kanisa la kwanza lilimtegemeza Paulo wala si mara moja, Fil 4:16 Usiwe na siku maalumu tu ya kutegemeza, lakini iwe ni kawaida kwako. Kutegemeza ni utii wa Neno la Mungu.