У нас вы можете посмотреть бесплатно MUBASAHARA (LIVE) KUPITIA TBC или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Itaka, Kanali Gelvas Chitola, amezungumza mubashara (live) kupitia chombo cha Habari cha Taifa TBC, akiwa katika eneo la Kimondo, Kata ya Ndolezi, Wilayani Mbozi. Akizungumza katika mahojiano hayo, Kanali Chitola ameeleza kuhusu mafunzo ya uzalendo na uzalishaji yanayotolewa katika Kikosi cha JKT Itaka, akibainisha kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea vijana nidhamu, uzalendo kwa Taifa pamoja na kuwapa ujuzi wa uzalishaji mali ili waweze kujitegemea. Amesema kupitia mafunzo hayo, vijana hupata fursa ya kujifunza stadi mbalimbali za kazi pamoja na kushiriki katika shughuli za uzalishaji zinazochangia maendeleo ya Taifa na jamii kwa ujumla. Aidha, amesisitiza kuwa JKT itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha vijana wengi zaidi wanapata mafunzo hayo muhimu kwa ajili ya kujenga Taifa lenye vijana wenye maadili, uzalendo na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.