У нас вы можете посмотреть бесплатно MAUAJI YA MTOTO MBEYA, POLISI WAMDAKA MWANAMAMA KWA TUHUMA ZA KUMUUA MTOTO WA JIRANI YAKE или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
ADAIWA KUMUUA MTOTO WA JIRANI YAKE (12) AKIMTUHUMU KUIBA MAYAI. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Furaha Mwile Nyelele, mkazi wa Kijiji cha Shilanga Mbeya vijijini kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa jirani yake aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Shilanga darasa la saba aitwaye Boniventure Elia Lazaro [12] mkazi wa Shilanga. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amesema mnamo Desemba 21, 2025 majira ya saa kumi jioni huko katika Kijiji cha Shilanga, Kata ya Ilembo, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Mbeya mtuhumiwa Furaha Mwile Nyelele alimpiga kwa kipande cha mti kichwani mtoto Boniventure Elia Lazaro (marehemu) na kumsababishia jeraha ambapo alikimbizwa katika Hospitali Teule ya Ifisi mjini Mbalizi kwa ajili ya matibabu. Hata hivyo Kamanda Kuzaga ameeleza kuwa ilipofika tarehe Desemba 22, 2025 saa sita mchana mtoto huyo akiendelea kupatiwa matibabu Hospitalini hapo (Ifisi) alifariki Dunia. Amesema kutokana na uchunguzi wa awali imebainika kuwa chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa huyo kujichukulia sheria mkononi baada ya kumtuhumu mtoto kuwa ameiba mayai ya kuku. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi ili kuepuka madhara huku likiwahimiza na kuwaasa wazazi na walezi kuzingatia suala la ulinzi na usalama wa mtoto kwa kuhakikisha haki za mtoto zinaheshimiwa na kulindwa ipasavyo.