У нас вы можете посмотреть бесплатно RC SENDIGA “UNA VIKOBA NANE, UTAMPA MUMEO KISUKARI” “TENDO LA NDOA HAWEZI UNAENDA KWA BODABODA” или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga amewataka Wanawake wakiwemo Viongozi kufahamu nafasi zao kwenye ndoa pindi wakiwa majumbani kwakuwa Mwanamke kufahamu haki yake haimaanishi aache kumuheshimu Mumewe na kuota masharubu akisema Wanaume wanahitaji kutunzwa pia. RC Queen amesema hayo jana Februari 03, 2026 wakati akiongea na Jumuiya ya Wanawake wa CCM Mkoani humo ikiwa ni mwendelezo ya maadhimisho ya miaka 49 tangu kuzaliwa kwa CCM ambapo amesema hadi sasa Mkoa wa Manyara una kesi zaidi ya 80 za vitendo vya ukatili wa kijinsia. “Wakina Mama amkeni na kufahamu nafasi zenu na thamani zenu, Mwanamke kufahamu haki yako hakumaanishi usimuheshimu Mumeo, hiyo ndio changamoto nyingine wakina Baba wanajua akina Mama wakijitambua ndani ni moto, tukisimama hapa sisi ni Viongozi tukirudi ndani sisi ni Wake na akina Mama wa Familia lazima tujue kucheza na nafasi hizo mbili” “Kuna muda mwingine tunapata matatizo kwasababu ya sie kujifanya tuna masharubu ndani, ndani ya nyumba mwenye sharubu ni mmoja, tunapodai haki zetu na sisi tutumize haki zetu nyumbani kama akina Mama, Mama tangu asubuhi kiguu na wewe miguu inanukia kama mbuzi anayechomwa” “Akina Baba nao wana mioyo wanataka kutunzwa, wewe muda wa kutunza Mume hauna muda wa ktunza Watoto hauna tukusaidie vipi?, Mama una vikoba nane huna sehemu ya kupata pesa unamtia Mumeo sukari bure tendo la ndoa ndani hawezi unakwenda kwa Vijana wa Bodaboda, ukija hapa pepeta nyumbani kuwa zuzu ndivyo mahaba yanavyotaka mahaba hayataki kelele”