У нас вы можете посмотреть бесплатно NDOA YAVUNJWA MAHAKAMANI, MKE NA MUME WAKUBALIANA KUSAKA WATOTO NJE YA NDOA "NIPO SINGLE" или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mahakama ya Mwanzo Buguruni imevunja ndoa ya wanandoa Raymond Kulaya (44) na Magreth Silaeli (37) waliotengana kwa miaka 10 baada ya kukubaliana kila mtu akatafute watoto “anapopajua” baada ya kuishi miaka mitano bila kupata mtoto. Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Matrona Luanda ambapo amesema mahakama hiyo iliangalia viini vikuu vitatu ikiwemo kama ndoa ya wawili hao ni halali baada ya kutengana tangu mwaka 2011. Katika hukumu hiyo, Hakimu Luanda amesema mahakama imepewa mamlaka ya kuvunja ndoa chini ya Kifungu cha 110 cha Sheria ya Ndoa. "Kwa mujibu wa Kifungu cha 107 kidogo cha 2 (f) mahakama hii inavunja ndoa ya wadahawa kwa kuwa walikiri kukubaliana kuacha na kila mmoja kwenda kutafuta watoto anapopataka, pia hawana watoto wala mali," Baada ya kusema hayo, Hakimu Luanda amesema haki ya kukata rufaa kwa mdaiwa ipo wazi. Katika kesi hiyo Magreth aliiomba mahakama hiyo itoe hati ya talaka, ili aweze kuolewa na mwanaume anayeishi naye, baada ya kutengana kwa muda na Kulaya. Wawili hao walifunga ndoa ya Kikristo na Kulaya mwaka 2006 mkoani Kilimanjaro na waliishi pamoja kwa miaka mitano bila kupata watoto. Magreth alidai wakati anaolewa na Kulaya alimkuta tayari na watoto wawili, lakini katika kipindi chote walichoishi pamoja hawakubahatika kupata watoto. Alidai mwaka 2011 mume wake alimueleza kuwa wamekaa kwa muda mrefu bila ya kuwa na watoto na kumwomba watengane ili kila mtu aende akatafute watoto. Alidai katika kipindi walichoishi pamoja, familia ya ndugu wa mwanaume ilikuwa inawasumbua kuhusiana na watoto na kuwasababishia kukosa raha. Aliiambia mahakama kuwa kutokana na kutopata mtoto, Kulaya alimweleza kuwa ni bora kila mtu aende upande mwingine kwani atakapoleta mwanamke mwingine ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja hataweza kumuelewa. Magreth alidai yeye na Kulaya walitengana kwa makubaliano hawakuwahi kuwa na ugomvi na sababu kubwa ya kutengana ilikuwa kukaa muda wa miaka mitano bila ya kupata mtoto.