У нас вы можете посмотреть бесплатно FAMILIA YA MAREHEMU JOKHA YATOA WITO WA HAKI KUFUATIA VIDEO ILIYOSAMBAA BAADA YA AJALI YA MIGOMBANI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mtazamaji wa Asam Online TV, utakumbuka kuwa mnamo tarehe 30 Septemba, kulitokea ajali mbaya ya gari katika maeneo ya Migombani, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, ajali ambayo ilisababisha vifo vya watu watatu, akiwemo marehemu Jokha Azizi Ghalib. Baada ya ajali hiyo, video mbalimbali zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, zikimuonyesha marehemu akiwa katika sehemu ya kuhifadhia maiti, huku mtu anayedaiwa kurekodi video hiyo akitamka maneno yasiyofaa na yenye kuudhi, jambo lililoibua masikitiko makubwa kwa jamii. Familia ya marehemu Jokha imejitokeza na kuomba mamlaka husika kuchukua hatua kali dhidi ya wale wote waliohusika na tukio hilo, wakieleza kuwa kitendo hicho kinakiuka misingi ya utu, maadili na haki za binadamu. Familia hiyo imesisitiza kuwa heshima kwa wafu ni jambo la msingi katika jamii, na kwamba watu wote wanapaswa kutumia mitandao ya kijamii kwa uwajibikaji na uadilifu, badala ya kudhalilisha marehemu na kuumiza wafiwa. #AsamOnlineTV #Migombani #AjaliZanzibar #HakiKwaJokha