У нас вы можете посмотреть бесплатно RAIS MWINYI AJUMUIKA FUTARI NA WANANCHI WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika futari ya pamoja aliyowaandalia. Hafla hiyo imefanyika leo, tarehe 12 Machi 2026, katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi. Akitoa shukrani kwa niaba ya waumini wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Maalim Mkashari amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa wema anaowaonesha wananchi wake. Amesema kiongozi mwema ni yule anayejali na kutenda mema kwa anaowaongoza, akisisitiza kuwa kufutarisha ni kitendo adhimu chenye baraka na thawabu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Naye Mkuu wa Wilaya ya Wete, Abdalla Ali Rashid, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa juhudi zake za kuimarisha huduma za kijamii katika mkoa huo pamoja na kudumisha amani nchini, hatua inayochangia kuwaunganisha wananchi. Wakati huo huo, Rais Dkt. Mwinyi amemtembelea Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mberwa Hamadi Mberwa, nyumbani kwake katika eneo la Limbani, Wete, kwa lengo la kumjulia hali. #ASAMOnlineTV #Zanzibar #Ramadhani #FutariYaPamoja #Pemba