У нас вы можете посмотреть бесплатно Ccm yaibuka mshindi wa Ubunge,Upinzani wabwagwa Arumeru Mashariki. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Msimamizi wa #Uchaguzi katika Jimbo la #Arumeru Mashariki Bwana Emmanuel Mkongo amemtangaza Mgombea wa #CCM Dr.John Palangyo kuwa amepita bila kupingwa kufuatia wagombea wengine kukosa sifa za kuteuliwa kuwa wagombea Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki. Akitoa matokeo ya Uteuzi huo Msimamizi Mkongo amesema tarehe31 march Mwaka huu Tume ya Taifaya Uchaguzi ilitangaza Jimbo la Arumeru Mashariki kuwa wazi kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mh.Joshua Nassari kukosa sifa za kuwa Mbunge wa Jimbo hilo. Baada ya kutangazwa uwepo wazi wa jimbo hilo, jumla ya fomo 11 zilitolewa kwa Wagombea wa vyama vya siasa 11 vilivyojitokeza kuwania kugombea Ubunge katika jimbo hilo na baada ya uchambuzi wa fomu hizo, wagombea 3 hawakuteuliwa kwasababu hawakurudisha fomu, wagombea hao ni kutoka chama cha Wananchi CUF, Chama cha DP na Chama cha TLP. Aidha Fomu za Wagombea wengine 7 zilirudishwa na zilionekana kuwa na mapungufu ya kisheria, fomu hizo ni za Mgombea wa Chama cha SAU wadhamini hawakufikia 25 hivyo kushindwa kukidhi matakwa ya kisheria, pia Mgombea hakulipa dhamana ya Tsh. 50,000/=, Mgombea mwingine wa Chama cha UPDP hakuwasilisha picha na hakulipa dhamana ya Tsh. 50,000/=, Mgombea mwingine ni kutoka Chama cha ADA –TADEA ambaye hakulipa ada ya dhamana ya Tsh. 50,000, mwingine ni AAFP hakulipa dhamana ya Tsh.50,000 na hakuwasilisha tamko la kisheria lililosainiwa na mwanasheria. Mgombea wa NRA hakuteuliwa kutoakana na kutowasilisha tamko la Kisheria, pia hakulipa dhamana ya Tsh.50,000/= Mgombea wa sita bw. Kawishe hakuwasilisha tamko la kisheria na kulipa dhamana ya Tsh. 50,000/= na Mgombbea wa Saba wa Chama cha DEMOKRASIA Makini hakuwasilisha idadi ya wadhamini 25 waliomo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Kufuatia matokeo hayo Mgombea wa Chama cha Mapinduzi amepita Bila Kupingwa.