У нас вы можете посмотреть бесплатно MISSENYI YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MIAKA 10 MFULULIZO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwasa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo. Akizungumza katika Baraza maalum la Madiwani la Kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) lililofanyika katika Ukumbi wa William F. Katunzi uliopo Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi leo Juni 17, 2025, Mhe. Hajjat Fatma Mwasa amesema ana kila sababu ya kuipongeza Missenyi kwa kupata hati safi miaka 10 mfululizo. "Nina kila sababu ya kuwapongeza kwa kupata hati safi kwa miaka 10 mfululizo, lakini sio tu kupata hati safi, mmepata hati safi kwa miaka 10 mfululizo mkiwa na hoja chache na zinazoelezeka, hii nayo imeleta faraja kubwa", amesema Mhe. Mwasa. Aidha, amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Mwenyekiti wa Halmashauri, Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji na Wataalamu wa Halmashauri kwa kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja. "Nimpongeze Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wetu na Wataalamu wetu, matunda yanayotokea Missenyi yanatokana na nguvu ya pamoja, yaani vile utendaji kazi mlionao, ushirikiano na kila kitu, hayo ndio yanayoleta matokeo chanya Missenyi", ameongezea Mhe. Mwasa. Awali akisoma taarifa fupi ya utekelezaji wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bw. John Paul Wanga amesema kwamba kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 Wilaya ya Missenyi imepata hati safi. Pia, amebainisha kwamba taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imejumuisha hoja za mwaka wa fedha 2023/2024, hali ya utekelezaji wa hoja za miaka ya nyuma kufikia mwaka wa fedha 2022/2023 pamoja na maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAC). Ambapo amefafanua kuwa, katika mwaka wa fedha 2023/2024, hoja 15 ziliibuliwa na kutolewa mapendekezo, kati ya hoja ziliibuliwa na kutolewa mapendekezo, hoja 10 zimejibiwa kikamilifu na kufungwa na kusalia hoja 5 ambazo ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Kusoma taarifa hii kwa undani zaidi, tembelea tovuti yetu www.missenyidc.go.tz