У нас вы можете посмотреть бесплатно Salama Na DEO GRATIUS SE6 EP64 | PRIVILEGED?! PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 Deo Gratias, jina tu linatosha kujielezea kama wewe nawe utakua kama mimi wa kutaka kujua maana ya majina ya watu ili uweze kujua tabia zao au ujiulize wazee wake walikua wanafikiria nini wakati wanaamua kumpa jina hilo mtoto wao. Kwa Deo maana imejibeba na imejikamilisha na kwa yeye kuamua kubaki na jina lake hilo hilo mpaka kwenye stage ambako ndo sehemu yake ya kazi inabidi hilo nalo likuambie jambo kuhusu yeye na jinsi ambavyo anajichukulia na kuyachukulia mambo ambayo ameyachagua kuyafanya. Shukrani ziende kwa Mungu ndo maana ya jina lake, shukrani ziende kwa Mungu kwa kila alifanyalo leo, shukrani ziende kwa Mungu maana baada ya wazee wake kumsomesha kwenye shule ambayo walikua wameianzisha wao na kuhakikisha kijana wao anapata elimu ambayo anastahili lakini yeye akaamua kuiacha fani ambayo aliisoma na kuamua kuwa mchekeshaji basi nadhani Shukrani ziende kwa Mungu, Shukrani ziende kwa Mungu kwa wazazi wake kuelewa, Shukrani pia ziende kwa Mungu kwasababu mwanga umeanza kuonekana kwenye lile alifanyalo sasa. Yeye na rafiki zake ambao ni vijana wenzake wamejikusanya na kuanzisha kundi lao linaloitwa Watu Baki, ila hawakuamka tu wakaanzisha, kuna ka story hapo nyuma yake ambapo ndo panaleta maana kwenye maisha yetu na yao kama watafutaji. Deo anakumbuka audition ya kwanza ya Stand Up Comedy ambayo aliwahi kuifanya na akashinda huko Mbagala, chini ya shindano lililokua likisimamiwa na Evans Bukuku, Deo anakumbuka kushinda MILIONI nadhani kwenye shindano hilo ingawa alipofika home aligundua kuna mwana alichomoka na elfu kumi yake, yaani kuna mwana alimuangalia Deo, kisha akakiangalia kibunda alafu akasema nah, hawezi kumpa yote lol. Courage ya kufanya mengine mengi ikiwa na pamoja na ambayo yanaendelea leo ilianzia hapo. Mengine yakabaki story! Story ya kujikusanya na wanae enzi za Cheka Tu na baadae kuamua kundoka na kuanzisha WatuBaki ilikua mmoja inabidi awe na uthubutu na uthubutu huo uliwezekana na mpaka leo wamesimama na wana time yao kwenye DSTV ambayo inatoa burudani nzuri tu kwa watu wao na vile vile bado matamasha ya nje wanafanya wao kama wao. Kwa wengi ikiwa pamoja na mimi tulipewa story kwamba Deo ni mtoto flani wa kishua alokua kutoka kwenye familia inayokula wali kwa kijiko na ndo maana baadhi ya mambo ilikua rahisi kwake kufanyika kwasababu ana uwezo wa kurudi nyumbani kwa Baba na Mama na akarudi na mzigo wa kutosha ambao unasaidia mambo yaende. Ila kwa mujibu wake, hiyo si habari na wala yeye hajatoka kwenye mazingira hayo ambayo wengi wanadhani ametokea. Bado safari ndo kwanza imeanza na kwa wenzake yeye akiwa kama kiongozi anaamini kama wakitulia pamoja na kufuata maono yao basi mengi mazuri tu yatakuja, ila sasa huo uwezo wa kuweza kutulia pamoja na kutengeneza kitu kikubwa na kizuri ndo inawezakana ikawa mtihani. Si wengi wameweza ingawa wapo ambao wameanza pamoja na mpaka leo wanaunguruma pamoja. Inawezekana na yangu matumaini wao pia wataendelea kuwa WatuBaki kwa muda wote ulobaki. Love, Salama. Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One The Incredible &... Follow: Twitter: / yahstonetown Instagram: / yahstonetown Facebook: / yahstonetown Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz