У нас вы можете посмотреть бесплатно MWANACHUO CBE AKUTWA AMEKUFA KWENYE DIMBWI LA MAJI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Mbeya, Tido Kadaga, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unaelea kwenye dimbwi la maji katika mtaa wa Miita Tano, kata ya Iganzo jijini Mbeya. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mbeya, Mrakibu Mwandamizi Malumbo Ngata, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa walipokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema majira ya saa nane mchana kuhusu uwepo wa mwili wa mtu kwenye dimbwi la maji eneo hilo. Amesema kikosi cha zimamoto na uokoaji kilifika eneo la tukio, kikafanikiwa kuutoa mwili huo, ambapo ilibainika kuwa ni mwanafunzi wa CBE kampasi ya Mbeya. Mwili wa marehemu umechukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya kwa ajili ya utambuzi zaidi na taratibu nyingine za kipolisi. Jeshi la zimamoto na uokoaji limeendelea kutoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari wanapokuwa karibu na maeneo yenye maji, hususani wakati wa msimu wa mvua, ili kuepusha ajali kama hizo.