У нас вы можете посмотреть бесплатно RC SENYAMULE; SERIKALI INAENDELEA KUKUZA KILIMO HAI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema Serikali inaendelea kuunga mkono juhudi za taasisi mbalimbali zinazohamasisha kilimo hai ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kulinda mazingira. Kauli hiyo imetolewa katika chakula cha jioni kilichoandaliwa Machi 5, 2026, ikiwa sehemu ya kufunga mkutano wa siku tatu wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM) na kufanyika katika ukumbi wa Hotel ya Midland Jijini Dodoma, kwa lengola kubadilishana uzoefu na kujadili maendeleo ya kilimo ekolojia hai Nchini. Amesema Serikali pia imeweka mazingira rafiki kwa wadau wa sekta hiyo, ikiwemo kutenga eneo kwa ajili ya kituo cha mafunzo ya kilimo kitakachosaidia kuwajengea uwezo wakulima na wadau wengine. “Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhamasisha kilimo hai ambacho kinasaidia kulinda mazingira na kuongeza tija kwa wakulima,” amesema Mhe. Senyamule. Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Peter L. M. Msoffe amesema matumizi sahihi ya mbinu za kilimo ekolojia hai yanasaidia kutunza rutuba ya udongo, kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza usalama wa chakula na lishe, hususan kwa wanawake wanaohusika zaidi katika shughuli za kilimo. Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TOAM, Bw. Bakari Mongo, amesema mkutano huo umewakutanisha wadau wa kilimo ekolojia hai ili kujadiliana na kushirikishana mbinu bora zitakazosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao huku wakilinda mazingira. Washiriki wa mkutano huo pia walifanya ziara ya mafunzo katika eneo la Bihawana kujionea utekelezaji wa mbinu za kilimo hai mashambani.