У нас вы можете посмотреть бесплатно Ukombozi Kupitia Unyang'anyaji, Siyo Uangamizi | Lesson 5 || 28 October 2025 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mungu hakukusudia kuangamiza Wakanaani, bali kuwanyang’anya nchi yao kwa haki ya kiungu (Kut. 23:28–30; 33:2; 34:11; Hes. 33:52; Kumb. 7:20). Lengo halikuwa mauaji bali utakaso wa nchi na ukombozi wa historia. Israeli waliitwa kubomoa madhabahu na sanamu zilizokuwa chanzo cha maovu (Kut. 34:13; Kumb. 7:5; 12:2–3), siyo kwa tamaa ya utawala, bali kuondoa sumu ya ibada ya sanamu. Wale waliotambua ukuu wa Mungu, kama Rahabu (Yosh. 2:9–14), walipokea rehema. Lakini waliokataa toba na kufunga mioyo yao kama Farao walijitenga wenyewe na rehema ya Mungu (Yosh. 11:19–20). Kwa hiyo, vita hivyo havikuwa uharibifu wa binadamu, bali vita vya utakaso—mchakato wa Mungu wa kuondoa giza lililoingia ndani ya ulimwengu Wake. Vivyo hivyo leo, Mungu anatuita kung’oa ndani yetu tabia na desturi zinazopinga utakatifu Wake, ili tuishi maisha ya ukombozi wa kweli. Tembelea Maisha-Kamili.com kwa masomo zaidi kuhusu mpango wa Mungu wa kuondoa uovu na kurejesha uhalisia wa maisha. Maisha Kamili: Twakufungulia Biblia, Uyaone Maisha. #Ukombozi #MunguHakimu #Utakaso #HakiNaAmani #MaishaKamili #BibliaHai #VitaVyaKiroho #RehemaNaHukumu