У нас вы можете посмотреть бесплатно HII NDIYO NJIA YA KUREJESHA AMANI KATIKA JAMII ZETU: KHUTBA YA IJUMAA / SHEIKH ABDULQADIR AL-AHDAL или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Majadiliano yanayozingatia adabu ni ufumbuzi wa migogoro Rais wa taasisi ya Al-Hikma Foundation, Sheikh Sharif Abdulqadir Al-Ahdal katika 'khutuba' ya Ijumaa aliyoitoa leo Novemba 21, 2025 katika Msikiti wa Nurul-Hikma ulioko Temeke, amehimiza jamii ya Watanzania kujenga utamaduni wa majadiliano yenye adabu, hekima na heshima kwa lengo la kulinda amani na mshikamano wa taifa. Katika khutuba yake iliyokuwa na kichwa cha habari, 'Adabu za majadiliano' Sheikh amesema hakuna binadamu aliyekamilika, na kwamba tofauti za kimitazamo au migogoro ni sehemu ya maumbile ya mwanadamu, jambo linalojitokeza hata katika familia na kati ya jamii mbalimbali. Akinukuu Qurani Tukufu, Sheikh Abdulqadir ameeleza kuwa Nabii Adamu (AS) alipokosea mbele ya Mola wake alikiri kosa na kutubu, na kwa sababu hiyo akapewa msamaha. Kinyume chake, Ibilisi (shetani) alikataa kukubali kosa na akaonyesha kiburi, hali iliyosababisha kulaaniwa. Amesisitiza kuwa katika Uislamu, watu wanapokosana au kutoelewana, wanahimizwa kukaa pamoja na kufanya majadiliano kwa lengo la kurejesha maelewano na ni vyema mwenye makosa akakiri kwa maslahi ya amani. Sheikh huyo amebainisha kwamba historia ya taifa inaonesha wazi namna wananchi walivyopambana na wakoloni hadi kupata uhuru, kisha kuendelea kujenga miundombinu na maendeleo mbalimbali ambayo yanapaswa kulindwa. Amefafanua kuwa miongoni mwa adabu muhimu za mazungumzo katika kusaka maelewano ni kutouona upande mwingine katika meza ya mazungumzo kuwa duni. Adabu nyingine muhimu amesema ni pamoja na kuweka mbele maslahi ya jamii badala ya maslahi ya chama, kabila au dini. Ameongeza kuwa kuzungumza kwa lengo la kutafuta amani haina maana ya udhaifu, bali ni alama ya busara. "Kufanya mazungumzo haina maana kwamba wewe ni dhaifu na si kwamba wewe umeshindwa bali inaonesha wewe una akili nzuri na hekima," amesisitiza. Sheikh Abdulqadir amesema hata katika Qurani, Mwenyezi Mungu alifanya mazungumzo na Malaika kabla ya kumuumba mwanadamu, jambo linaloonesha kuwa mjadala una nafasi muhimu katika kutafuta haki. Akimalizia khutuba yake amewataka vijana kuepuka maneno ya chuki na kusikiliza ushauri wa wazee na viongozi wa dini kwa ajili ya kulinda amani ya nchi yao.