У нас вы можете посмотреть бесплатно MAKONDA AELEZA DHAMIRA YA KUGOMBEA UBUNGE ARUSHA MJINI "NIMEITWA KUTUMIKIA WANANCHI” или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda, ametangaza kwa moyo wa unyenyekevu dhamira yake ya kuwania ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, akieleza kuwa ni muda sasa wa kuisuka upya Arusha na kuifanya kuwa ya mfano si tu kwa Tanzania bali Afrika Mashariki kwa ujumla. Akizungumza mbele ya viongozi mbalimbali wa dini katika, Makonda ameeleza safari yake ya kiuongozi iliyojengwa kwa kujifunza, kujitoa, na kuwa mtumishi wa watu katika nafasi tofauti alizowahi kushikilia—kuanzia uongozi wa serikali ya wanafunzi, umoja wa vijana, bunge la sheria, hadi kuwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, na hatimaye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa Mwenezi wa chama. Katika hotuba yake, Makonda ametaja sifa tatu kuu ambazo zimekuwa msingi wa mafanikio yake ya kiuongozi: Mahusiano bora, uwezo wa ushawishi, na kufikiri nje ya mipaka ya kawaida ambapo kupitia sifa hizo, Mkoa wa Arusha umeweza kushuhudia matukio makubwa yenye kuingiza kipato kwa wananchi na kuchochea maendeleo. “Nimejifunza kuwa uongozi si cheo, ni kujitoa. Ndiyo maana leo moyo wangu umeridhia kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Arusha Mjini. Nina maono ya kuibadilisha Arusha kuwa Taasisi ya mfano itakayojengwa juu ya misingi ya haki, ubunifu na huduma kwa wananchi,” amesema. Katika sera zake alizoziweka wazi, ameahidi kuibadilisha ofisi ya Mbunge kuwa Taasisi ya huduma kwa jamii, akieleza kuwa itakuwa na vitengo vitano vikuu, kikiwemo kitengo maalum cha sheria kwa ajili ya kutetea haki za wananchi wanyonge na mwananchi atakayeshindwa kumudu gharama za wakili, atagharamiwa na ofisi hiyo. “Kwa hiyo, kama ni kazi ninayo – ninachotafuta ni nafasi ya kuwatumikia wananchi,” amehitimisha kwa sauti ya matumaini. Baada ya kutoa tamko hilo, viongozi wa dini waliomzunguka wamemuombea kwa pamoja, wakimpa baraka na kumtakia mafanikio katika safari yake mpya ya kisiasa.#shortvideo #trendingshorts #trending