У нас вы можете посмотреть бесплатно Wawili waongezwa na kufika 27 KESI YA LOLIONDO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Watu wawili wameongezwa na kufika 27 katika kesi ya jinai namba 11 ya mwaka 2022 inayowakabili wananchi wa tarafa ya loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha wakikabiliwa na mashtaka mawili ikiwa ni nia ya kupanga njama za mauaji na jingine ni mauaji . Shauri hilo ambalo lilifikishwa mahakamani hapo kwaajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Herieth Mhenga wakili wa wa upande wa Serikali Upendo Shemkone ameiambia mahakama kuwa july 5 mwaka huu na kuomba kufanya mabadiliko yahati ya mashtaka kwa kuongeza washtakiwa wengine wawili na kufanya kuwa na washtakiwa katika shsuri hilo kuwa 27 na kuiomba mahakama hati hiyo iweze kusomwa kwa washtakiwa wote Ambapo upande wa Utetezi wakiongozwa na wakili Ally Myela walipinga kusomwa kwa hati hiyo kwa vigezo kwamba wateja wao hawakufikishwa mahakamani july 5 mwaka huu ambapo hati hiyo ilifanyiwa marekebisho kwa kuongeza washtakiwa hao wengine kitu ambacho ni kinyume na sharia na kuiomba Mahakam ikatae kutoa amri ya kusomwa kwa hati mpya ya mashtaka ikijumuisha washtakiwa wote 27 . Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Herieth Mhenga amesema kisheria yeye amefungwa mikono kwakuwa alishatoleauamuzi jambo hilo toka july 5 mwaka huu kuwa hati hiyo ipokelewe mahakamani na kuwataka mawakili wa utetezi kama hawajaridhika kwa namna yeyote na uamuzi huo wachue hatua ntingine za kisheria . Pia kulikuwa na hoja ya kuwa upelelezi haujakamilika na kuaomba shauri hilo liahirishwe na kupangiwa tarehe nyingine ambapo mawakili wa utetezi walilipinga tena vikali na kusema kwakuwa shauri lina mashtaka mawili shtaka la kwanza la kula njama ya mauaji na jingine la kuua ambapo katika shtaka la kwanza la kuapanga njama za kuua ni shtaka ambalo kimsingi mshtakiwa hawezi kufikishwa mahakamani kabla upelelezi haujakamilika . Ambapo mawakili hao walikuwa na hoja kwamba katika mahakama isiahirishe kesi katika shtaka la kwanza la kupanga njama za mauaji kwakuwa upelelezi wa shtaka hilo kuwa haujakamilika na kusema lazima utakuwa umekamilika ndio washtakiwa wakamatwe. Na mahakama kutoa amri ya july 28 itatoa uamuzi kama ni sahihi shtaka la kula njama kuendelea kuahirishwa mahakamani kwa kigezo cha upelelezi kutokamilika au laa na kukubaliana na upande wa mashtaka katika shtaka la pili la mauaji kuendelea na upelelezi kwakuwa inakuwa haivunji sheria kwakuwa inaruhusu upepelezi katika makosa kama hayo kufanyika bila ukomo . Huku hoja ya tatu ni kuzingatia haki Wagonjwa ambao ni mshtakiwa 22 anamatatizo ya figo 19 anahitaji uangalizi wa karibu kama dawa ,chakula mshakiwa namba 3 na 23 wakiwa ni Wanafunzi wanaoshtakiwa kwenye Shauri hilo hivyo ombi lao ni kuharakisha upelelezi . Hakimu anayesikiliza Kesi hiyo Heriet Mhenga ameahirisha shauri hilo mpaka july 28 mwaka huu na washtakiwa wote wamerudishwa lumande .