У нас вы можете посмотреть бесплатно EU kutoa Sh580 bilioni kutatua changamoto ya maji Mwanza или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kutokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika jiji la Mwanza na maeneo jirani, Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) imepanga kutoa zaidi ya Sh580 bilioni sawa na Euro 200 milioni kufadhili utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa chanzo na kituo cha tiba ya maji Butimba jijini Mwanza, ili kuongeza uzalishaji wa maji na kukidhi mahitaji. Awamu ya kwanza ya mradi huo uliogharimu zaidi ya Sh70 bilioni ilikamilika Desemba, 2024 na imeanza kutoa huduma kwa kuongeza uzalishaji wa lita milioni 48 kwenye usambazaji wa maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (Mwauwasa). Kwa sasa mahitaji ya huduma ya maji katika jiji la Mwanza ni lita milioni 172 huku uzalishaji uliopo ni lita milioni 138, hivyo kuwapo na wa takribani lita milioni 34. Akizungumza jijini Mwanza baada ya kutembelea na kujiridhisha na ufanisi wa mradi wa maji Butimba, Mkuu wa Mashirikiano wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Marc Stalmans amesema lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa kuongeza uzalishaji mara tatu ya sasa. Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (Mwauwasa), Nelly Msuya ameeleza hali ya upatikanaji wa maji na umuhimu wa mradi huo kwa ukuaji wa jiji hilo, huku Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mwanza anayesimamia Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Patrick Karangwa akiipongeza jumuiya hiyo kwa kuunga mkono miradi ya Serikali. (Imeandikwa na Damian Masyenene)