У нас вы можете посмотреть бесплатно MAUAJI MGODINI TARIME или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mtu mmoja anayedaiwa kuwa miongoni mwa wavamizi kwenye mgodi wa dhahabu wa African Barrick North wilayani Tarime ameuawa baada ya kupigwa risasi na mlinzi wa mgodi huo aliyekuwa akijihami. Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Tarime na Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi Justus Kamugisha, amemtaja mtu aliyeuawa kwa kupigwa risasi moja chini ya bega la mkono wa kushoto kuwa ni Joseph Mwikwabe mkazi wa kijiji cha Kwisarara kata ya Bumera wilayani humo. Mwili wa marehemu Joseph Mwikwabe, bado umehifadhiwa katika mochwari ya hospitali ya wilaya ya Tarime ukisubiri daktari wa familia kuufanyia uchunguzi. Kamanda Kamugisha amewataka wananchi kuacha tabia ya kuvamia ndani ya mgodi huo kwa ajili ya kuiba mawe ya dhahabu. Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi zaidi ya watu 30, wanaoaminika kuwa ni wavamizi walikutwa na walinzi wanne wa mgodi huo wakiwa ndani ya shimo la Gokona na walipoamriwa waondoke walikaidi amri na kuanza kuwashambulia kwa silaha mbalimbali za jadi huku wakiwarushia mawe, hali iliyomfanya mmoja wa walinzi hao Steven Kawanga kujihami kwa kufyatua risasi iliyomjeruhi marehemu na hatimaye kufariki dunia. ---------------------------------