У нас вы можете посмотреть бесплатно Huduma ya Tiba Saidizi kwa uraibu wa afyuni Nafasi ya Asasi za Kiraia или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
ISSUP Tanzania, inaandaa semina mtandaoni kuhusu Tiba Inayosaidiwa na Madaktari kwa Matatizo ya Matumizi ya Opioidi: Nafasi ya Mashirika ya Jamii ya Kiraia Webinar hii itashirikisha uzoefu wa utoaji tiba saidizi kutokana na matumizi ya dawa za kulevya, ikionyesha nafasi ya Asasi za Kiraia (CSOs) na Serikali nchini Tanzania. Lengo ni kuelezea jinsi CSOs zinavyotoa huduma za rufaa kwenye tiba saidizi kwa watu wenye uraibu wa afyuni, na jinsi Serikali inavyoratibu, kusimamia, na kusaidia juhudi hizi ili ziendane na sera na mikakati ya kitaifa. Matokeo ya kujifunza: Malengo ya Kujifunza ni pamoja na: Kuelewa dhana ya tiba saidizi na umuhimu wake katika kushughulikia changamoto za matumizi ya dawa za kulevya jamii ya afyuni Kutambua nafasi na majukumu ya Asasi za Kiraia (CSOs) katika utekelezaji wa huduma za tiba saidizi ngazi ya jamii Kupata uelewa wa jukumu la Serikali katika kuratibu, kusimamia, na kusaidia afua za tiba saidizi Kujifunza kutoka kwa uzoefu halisi na masomo yaliyojifunzwa katika utekelezaji wa huduma za saidizi nchini Tanzania Kubaini changamoto za utekelezaji na mbinu zilizotumika kuzitatua Presenters: Deogratius Ramale Head, Training and Development, ISSUP Tanzania Expertise – Psychologist, Master Trainer for UTC and UPC. Marineus Mutongore Chairperson of the Key and Vulnerable Populations (KVP) Forum Tanzania Ex-drug user Damali Kabwali Head of Programs, Tanzania Network of People who Use Drugs (TANPUD). Member – ISSUP Tanzania. Said Bandawe Executive Secretary, Gift of Hope Foundation. Member, ISSUP Tanzania. Peer Recovery Support Professional, Ex-Drug User . Surah Nyembo Director, Drug Abuse Prevention Organization (DAPO). Member, ISSUP Tanzania. Peer Recovery Professional, Ex-Drug User. Moderator: Shabani Miraji Prevention Officer, Drug Control and Enforcement Authority (DCEA). Educational Psychology, Master Trainer for UPC. Semina za mtandaoni na matukio ya mtandaoni yanayotolewa na kuandaliwa na Chama cha Kimataifa cha Wataalamu wa Matumizi ya Dawa za Kulevya (ISSUP) yanatolewa kwa madhumuni ya taarifa pekee. Ni ya kielimu kwa asili na hayahusishi ushauri wa matibabu, utambuzi au tiba. Webina hii ilirekodiwa tarehe 10 Machi 2026