У нас вы можете посмотреть бесплатно LUSINDE ALIA WANAOOMBA AJIRA KUFANYIWA MITIHANI, ATOA PENDEKEZO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mbunge wa Mvumi (CCM), Livingstone Lusinde amekosoa utaratibu wa waajiriwa wapya kufanyiwa mtihani kabla ya kuajiriwa na badala yake ametaka vitumike vyeti. Lusinde ameyasema hayo leo Jumatatu Aprili 14, 2025 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2025/26. Makadirio hayo yaliwasilishwa Aprili 9, 2025 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiomba Bunge limuidhinishie Sh782.08 bilioni. Akichangia mjadala huo, Lusinde amesema kama Serikali inaona hawawezi kuajiri Watanzania wote kwa kutumia ajira kupitia mfumo wa ajira wa portal, basi zigawanywe katika kila halmashauri. Amesema endapo halmashauri hawatapata watu wenye elimu inayohitajika basi watazirudisha katika mikoa mingine ili waweze kuajiriwa. “Huu utaratibu wa kuwaleta pamoja, hivi vyeti mlivyowapa mnavikagua unasema hiki ni cheti chako original (halisi) kabisa halafu baadaye unamuingiza katika mtihani wa dakika moja ndio umkoseshe mtoto ajira, haiwezekani,” amesema. Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi