У нас вы можете посмотреть бесплатно ZANZIBAR YAENDELEA KUVUTIA WATALII, WANAMAZINGIRA WAANDAA USAFI WA PWANI KILIMANI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Zanzibar ni kisiwa chenye mvuto wa kipekee barani Afrika, kikijulikana kwa historia yake adimu, mandhari ya kuvutia na utamaduni wake wenye haiba maalum. Ni miongoni mwa maeneo ambayo watalii hupendelea kutembelea kwa ajili ya kupumzika kutokana na uzuri wa fukwe zake, mazingira tulivu na ukarimu wa wenyeji. Serikali ya Zanzibar imeendelea kuimarisha sekta ya utalii kupitia maboresho ya miundombinu, kampeni za kimataifa za kutangaza vivutio vyake, pamoja na kuhifadhi maeneo muhimu ya kihistoria na kiasili. Hatua hizi zinalenga kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi. Bahari ikiwa ni moja ya rasilimali kuu za vivutio vya utalii Zanzibar, inalazimu kulindwa na kutunzwa kwa uangalifu ili mazingira yaendelee kuwa safi, viumbe wa majini walindwe, na rasilimali hiyo iendelee kunufaisha jamii na wageni kwa vizazi vijavyo. Katika kuunga mkono juhudi hizo, wanajumuiya wa Mnara Wambao Environmental Conservation kutoka Botanic Garden Migombani wameandaa programu maalum ya usafi katika pwani ya Kilimani. Zoezi hilo linatarajiwa kuboresha mazingira ya bahari, kulinda mikoko na kuongeza uhamasishaji kwa wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira ya baharini. Juhudi hizi zinaakisi dhamira ya pamoja ya kuhifadhi kivutio hiki muhimu ili Zanzibar iendelee kuwa miongoni mwa visiwa bora zaidi duniani kupendeza watalii.