У нас вы можете посмотреть бесплатно ZECO YAFANUA SABABU ZA KUKATIKA UMEME MARA KWA MARA ZANZIBAR или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kukatika kwa umeme mara kwa mara visiwani Zanzibar kunatokana na ongezeko la miradi mikubwa ya uwekezaji inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali, hali inayosababisha shinikizo kwenye mfumo wa upatikanaji wa umeme na wakati mwingine kusababisha umeme kuzimwa bila mpangilio maalumu. Hayo yameelezwa na Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Ndugu Haji Mohamed Haji, wakati akitoa maelezo kuhusu changamoto ya upatikanaji wa umeme inayojitokeza nchini, alipokuwa akizungumza ofisini kwake Malindi, Wilaya ya Mjini. Amefafanua kuwa ujenzi wa viwanda, viwanja vya michezo pamoja na miradi mingine mikubwa ya uwekezaji umeongeza mahitaji ya umeme, hali inayosababisha kupungua kwa nguvu ya upatikanaji wa umeme kwa wakati mmoja katika baadhi ya maeneo. Aidha, amesema kutokana na changamoto hiyo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandaa mpango wa kuboresha na kuimarisha matumizi ya betri maalumu za kuhifadhi umeme, hatua itakayosaidia kuongeza uthabiti wa huduma ya umeme na kuwezesha wananchi kupata umeme wa uhakika kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kwa upande wao, wananchi wameliomba Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kuboresha miundombinu ya umeme na kuweka utaratibu wa kutoa taarifa kwa wakati kuhusu sababu za kukatika kwa umeme, ili kuepuka usumbufu unaosababishwa na kuzimika kwa umeme bila taarifa.