У нас вы можете посмотреть бесплатно Hawatokuwepo Waislam wasio na Uislam - Sheikh Kilemile - Part 1 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kwa karne nyingi, Uislam hasa kwa nchi za Magharibi, umeendelea kuwa ni kikwazo kwa maslahi yao. Uliendelea kupigwa vita kwa muda mrefu mpaka walipofanikiwa kuivunja Dola ya Kiislam iliyokuwa na makao makuu yake hapo mjini Islambul uliobadilishwa jina na sasa kuwa Istanbul nchini Uturuki. Lengo kuu lilikuwa ni kuzinyakua rasilimali zilizoko katika nchi mbalimbali zikiwemo za kiislam. Waliamua kuigawa ardhi ya Dola ya kiislam vipande vipande vya nchi ndogo ndogo ambazo walipeana kuzitawala aidha moja kwa moja au kupitia viongozi wa kiislam walioko katika nchi hizo kama vibaraka wao. Kama hiyo haitoshi, na hasa baada ya kuona kwamba waislam licha ya kutawaliwa, bado wanao msimamo juu ya dini yao kutokana na kuizingatia Qur’an, juhudi zao zilianza kuelekezwa katika kuwafanya waislam wasiitekeleze Qur’an na hivyo kuwafanya wawe ni waislam majina tu, bila ya kuufahamu na kuufuata uislam unaotakiwa na Mwenyezi Mungu, kama ulivyoelezwa ndani ya Qur’an na katika ufafanuzi wa Mtume Muhammad (S.A.W) uliohifadhiwa ndani ya Vitabu vya Sunnah. Lakini kwa mujibu wa maelezo ya Sheikh Suleiman Kilemile, watu hawawezi kuitwa ni waislam wasipokuwa ni wenye kuyatekeleza yaliyomo kwenye Qur’an na katika Sunna za Mtume Muhammad (S.A.W). Sasa fuatana na Sheikh upate kuelimika zaidi kupitia Mada hii…