У нас вы можете посмотреть бесплатно WANANCHI WALIOBAKI NGORONGORO WAFANYA TUKIO KUBWA , WAPOTOSHAJI WABAKI MDOMO WAZI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#breakingnews #2gendahtvonline #ngorongoro Wananchi wa jamii ya kimasai wanaoishi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro wamefanya tamasha la kimila la kiutamaduni Katika tamasha hilo la kiutamaduni jamii hiyo kuanzia katika rika la ujana wakiongozwa na wazee waliweza kufanya matambiko ya kimila ndani ya kreta bila kubughudhiwa na mtu yoyote na kuelezwa kwamba tukio hilo hufanyika kila baada ya miaka kumi. Tazama Kwa kidogo wanavyosherekea Kwa uhuru wote. Kufanyika kwa tukio hilo la kimila ambalo kwa mujibu wa jamii ya kimasai hufanyika takribani kila baada ya miaka kumi limewavunja nguvu baaadhi ya mashirika yanayodai kutetea haki za binadamu kwani madai yao ya jamii hiyo kuzuiwa kufanya shughuli yoyote ndani ya hifadhi yanaonekana kuwa ni ya uongo. Mashirika hayo yamekuwa yakidai kwamba jamii ya wamasai nchini Tanzania imekuwa ikishurutishwa kuhama kutoka eneo hilo la tarafa ya Ngorongoro na kuhamia katika Kijiji cha Msomera na maeneo mengine yaliyotengwa na serikaii. Hata hivyo serikali ya Tanzania imekuwa ikipuuza tuhuma hizo ambazo mara nyingi zimekuwa zikitolewa na mashirika wanaowatumia jamii ya kimasai kama chanzo cha kupata fedha badala ya kujali maendeleo yao ya kila siku. Jamii ya kimasai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ikiishi katika maisha magumu kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanyama pori na hivyo kusababisha mauaji ya binadamu hasa Watoto wadogo na wanawake na hivyo kuhatarisha maisha yao, Serikali iliamua kuwahamisha kwa hiyari wananchi kutoka ndani ya hifadhi ili kuwanusuru na vifo vya mara kwa mara vinavyotokana na ongezeko kubwa la wanyama wakali linalochangiwa pia na ongezeko la idadi ya watu ambapo uamuzi huo kwa sasa umepunguza vifo vingi.