У нас вы можете посмотреть бесплатно MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI YAACHA MAAFA KILOSA, NYUMBA ZAIDI YA 120 ZAHARIBIKA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Morogoro: Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro imekumbwa na maafa baada ya nyumba kuezuliwa paa, kubomoka kuta na nyingine kubomoka kabisa kutoka na mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha Ijumaa Desemba 26, 2025 saa 10:30 alasiri hadi saa moja usiku, katika Tarafa ya Magole. Akizungumza leo Desemba 27, 2025, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, amesema mvua hizo ziliathiri zaidi maeneo ya Tarafa ya Magole katika kata za Dumila na Mgaole, ambapo kwa tathmini ya awali zaidi ya nyumba 120 zimepata madhara mbalimbali ikiwemo kuezuliwa paa, kuporomoka kwa kuta na nyingine kubomoka kabisa. Amesema kuwa takwimu hizo ni za awali na kamati ya maafa ya wilaya inaendelea na kufanya tathmini ya kina ili kupata idadi sahihi ya nyumba na wananchi walioathirika pamoja na kiwango halisi cha uharibifu uliosababishwa na maafa hayo. Imeandaliwa na Jackson John.